Johan Boje, msaidizi wa polisi wa Eneo la Kati na Magharibi mwa Jutland anafariki baada ya kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa kwa kasi akiwa nje ya nyumbani kwake usiku mmoja wa manane mwezi Machi. Bosi wake, Alex Borg, ni mmoja wa watu wa kwanza kufika kwenye eneo la tukio. Kwa haraka anagundua kuwa hii si ajali ya kawaida ya kugongwa na gari na kisha mtuhumiwa kuhepa, lakini ni mauaji ya kikatili. Mwanake Boje mwenye umri wa miaka tisa anadai kuwa aliliona gari hilo, na kwamba lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi. Je, ni fikra za kijana huyo mwenye mfadhaiko zinamchezea shere? Kamera ya uchunguzi ya kituo cha mafuta inathibitisha masimulizi ya mtoto – mtu fulani aliyekuwa amevalia sare za polisi alikuwa anaendesha gari hilo wakati wa usiku huo wa ajali ya mauti. Roland Benito, mpelelezi katika Mamlaka ya Malalamishi ya Polisi, anapewa usukani wa kuendesha kesi. Ni nani kati ya marafiki wa Johan Boje alikuwa na nia ya kutenda maovu kama hayo? Rolando Benito anaungana na Anne Larsen, mwanahabari kutoka kituo cha televisheni cha TV2 East Jutland. Wanafuatilia alama za magurudumu hadi kwenye moto, ambao ulikuwa na hasara kubwa kwa familia ya eneo hilo. Labda moto huo haukuwa ajali? Anne na Rolando wanakisia kuwa huenda nia ikawa ni tofauti sana na kile walichotarajia mwanzoni. Msako wa kumtafuta mhalifu huyo unaanza kabla hajafanya shambulizi lingine.